Jumanne, 3 Mei 2016

Maamuzi mapya ya TFF kuhusu kipa wa Simba aliyefungiwa miaka 10 kucheza soka



Baada ya April 3 2016 shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia kwa makamu mwenyekiti wake Jerome Msemwa waliamua kutangaza kutoa adhabu kwa viongozi, wachezaji na timu za Ligi daraja la kwanza zilizokuwa zinahusishwa timu za Kundi C katika upangaji wa matokeo.
TFF baada ya kupitia upya adhabu ilizotoa April 3 2016 imeamua kumfutia adhabu golikipa wa Simba aliyekuwa kwa mkopo katika klabu ya Geita Gold Denis Richardambaye awali alitangazwa kupewa adhabu ya kufungiwa miaka 10 kucheza soka na faini ya milioni 10 kutokana na kutuhumiwa kwa upangaji wa matokeo.
Denis Ricahard alipatikana na hatia baada ya kumuomba muamuzi ruhusa ya kwenda kujisaidia na kukaa muda mrefu bila kurudi, hivyo kwa mujibu wa makamu mwenyekiti wa kamati ya rufaa Revocatus Uhuri amemfutilia mbali adhabi hiyo na kusema refa ndio alishindwa kumudu mchezo.
Hata hivyo katika rufaa hiyo ni Denis Richard pekee aliyefutiwa adhabu, kama ulikosa waliopewa adhabu April 3 2016 Bonyeza HAPA
CHANZO : Salehjembe

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni